Rapper Rosa Ree kutoka Tanzania amewaponda watu maarufu ambao wanajitosa katika mziki kisa wana wafuasi wengi kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii.
Rosa Ree anawataka watu maarufu mitandaoni wenye tabia hiyo waelewe kwamba kuwa na wafusi wengi kwenye mitandao ya kijamii haimaanishi wanaokufuatilia watakua mashabiki wa mziki wako moja kwa moja.
Kulingana na Rosa Ree ni kwamba Tabia hii imechangia pakubwa kushuka kwa thamani ya mziki kwani Sanaa imevamiwa na watu ambao hawana vipaji.