Msanii Nyota Ndogo ameelezea kusikitshwa kwake na hatua ya mziki wake kutofanya vizuri kwa sasa katika soko la mziki licha ya kuwa na mashabiki wengi.
Akizungumza na Take over Nyota ndogo amesema inavunja moyo kuona kwamba licha ya kuwa na mashabiki Zaidi ya laki nne wanaomfuatilia kwenye mitandao tofauti bado wimbo wake wa mwisho una views 60000 tu kwenye mtandao wa youtube licha ya wimbo huo kutoka mwaka mzima uliopita.