Waumini wa kanisa moja eneo bunge la Bobasi huko kaunti ya Kisii wamepatwa na mshangao baada ya wezi kuvunja kanisa hilo, wakapika kabla kuiba vyombo vya ibada.
Kulingana na Kiongozi mmoja wa kanisa hilo kwa jina Tom Mosoba ni kwamba kinachowashangaza zaidi ni kwamba wezi hao walipika ndizi walizozipata ndani ya kanisa hilo na kuzila baada ya kuvunja na kuingia, kabla ya kutekeleza wizi.
Chifu wa eneo hilo anasema kwa sasa mshukiwa mmoja tayari amekamatwa na anasaidia polisi kwenye uchunguzi.