Wasanii wa mziki wa kizazi kipya kutoka kanda ya pwani wamepinga vikali madai kwamba walilipwa shilingi milioni 200 na serikali ya Mombasa katika tamasha la mziki la kufunga mwaka lililofanyika katika bustani ya Mama ngina wakati wafanyikazi wa kaunti ya Mombasa walikua hawajalipwa miezi 3 mfululizo.
Baadhi ya wasanii waliotumbuiza kwenye tamasha hilo wanadai kiwango wanachodaiwa kutumika katk auandalizi wa tamasha hilo sio cha ukweli na kinalenga kuiharibia jina serikali ya kaunti ya Mombasa.
Kwa upande wake mmoja ya waandalizi watamasha hilo msanii Susumila ameeleza kwamba wasanii waliotumbuiza katika tamasha hilo bado kufikia sasa hawajapokea malipo yao kamili kinyume na madai ya watu.