Mwanamziki wa nyimbo za injili Rose Muhando kutoka Tanzania amezua gumzo baada ya kusema kwamba amechoka kuwa single na anatafuta mme wa kumuoa.
Kupitia Instagram, Rose Muhando amesema kwamba anatafuta mume wa kumuoa na sharti la kwanza anafaa awe ni mzungu na kigezo cha pili awe na hela.
Itakumbukwa kwamba mwaka jana msanii huyo alinukuliwa akisema kwamba anafurahia saana kuwa single na hayuko tayari kuingia kwenye mahusiano yoyote.