Mwanamitindo Kylie Jenner kutoka nchini Marekani ametajwa kuwa mwanamke mwenye wafuasi wengi mtandao wa Instagram duninani.
Mrembo huyo ametajwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa na wafuasi zaidi ya milioni 303.
Duniani, anaeshikilia namba moja kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi katika mtandao wa Instagram ni mchezaji wa soka wa klabu ya Manchester United, Cristiano Ronaldo mwenye zaidi ya wafuasi Milioni 393 kwa sasa.