Msichana moja amezua gumzo katika mitandao ya kijiamii baada ya kufichua kuwa aliachwa na mpenzi wake miezi mitatu tu baada ya kumpatia figo lake.
Colleen Le kupitia akaunti yake ya TikTok, ameelezea jinsi alivyoachwa njia panda miaka sita iliyopita baada ya mpenzi wake kuchepuka na mwanamke mwengine mda mfupi baada ya kumpatia figo lake katika upasuaji.
Katika video hiyo ambayo imejipatia mamilioni ya watazamaji kufika sasa katika mtandao huo, Colleene amefichua kuwa kufikia sasa bado jamaa huyo anaishi kwa utegemezi wa figo lake.
@colleeeniie Everything happens for a reason 😬 #fyp #foryoupage #foryourpage #fypシ #kidneydonation #kidneydonor #relationshipgoals #relationships