Msanii kutoka kundi la mziki la P Square kwa jina Mr P kutoka Nigeria, ametoa wito kwa wanawake kote Afrika kujenga tabia ya kuwapa zawadi za gharama wapenzi wao siku ya Valentine.
Mr. P amesema kwamba wanaume pia wanahitaji zawadi za thamani kama vile majumba, magari na PS4 na sio boxer, soksi na mishipi ya suruale.
Kulingana na star huyo ni kwamba mara kwa mara wanaume wanafanya jitihada kuwafurahisha wapenzi wao ila kwa upande wao wanawake hawajarudisha mkono.