Msanii Chris Brown nchini Marekani anakabiliwa kesi ya mpya ya kumwelesha kabla ya kum’baka mwanamke mmoja katika jiji la Miami.
Mwanamke mmoja amefika mahakamani akitaka kulipwa dola za kimarekani milioni 20 baada ya msanii huyo kufanya mapenzi naye kwa ulazima walipokutana katika sherehe.
Mwanamke huyo anadai tukio hilo lilitokea tarehe 30 mwezi Disemba mwaka wa 2020 lakini aliogopa kujitokeza na kuripoti kisa hicho hadi majuzi na kufikia sasa kambi ya msanii Chris Brown bado haijatoa tamko lolote kuhusu madai haya.