Msanii Otile Brown amezua wasiwasi miongoni mwa mashabiki baada ya kutangaza kwamba ametoka kufanyiwa upasuaji hospitalini.
Otile brown amepachika picha katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha kwenye machela akitolewa chumba cha upasuaji hospitalini na kuelekezwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali moja jijini Nairobi.
Otile Brown hajatoa maelezea zaidi kuhusu ugonjwa unaomsumbua lakini amewasistizia mashabiki kwamba yuko salama na anaendelea vizuri.