Msanii Davido hatimaye ametekeleza ahadi yake ya kugawa utajiri wake kwa makao ya watoto mayatima nchini Nigeria aliyoitoa mwaka jana, baada ya mashabiki kumchangia pesa za birthday kufuatia ombi lake mtandaoni.
Davido ametoa milioni 250 pesa za Nigeria ambazo ni sawia na shilingi milioni 68 pesa za Kenya, kwa makao 290 ya mayatima katika miji tofauti nchini Nigeria.
Mwaka jana wakati wa siku yake ya kuzaliwa, Davido alifanikiwa kuchangisha Naira milioni 200 ambazo ni sawia na shilingi milioni 54 katika kipindi cha masaa 72, baada ya kutania mashabiki katika mtandao wa twitter kwamba alihitaji kuchangiwa fedha za kusherehekea birthday yake.