Home BURUDANI Msanii Ajiadhibu Baada Ya Kuchelewa Kufika Katika Show Uganda

Msanii Ajiadhibu Baada Ya Kuchelewa Kufika Katika Show Uganda

225
0

Msanii Pallaso kutoka nchini Uganda amezua gumzo baada ya kuamua kufagia mitaa na barabara kama njia mojawapo ya kuomba msamaha kwa kuchelewa kufika kwenye tamasha alilopaswa kutumbuiza.

Taarifa kutoka Uganda zinasema kwamba star huyo alifaa kutumbuiza katika mkahawa mmoja eneo la mji wa Masaka usiku wa jumatatu ya Valentine, lakini alichelewa kufika na kupelekea siku yake ya kutumbuiza kuahirishwa hadi usiku wa jana Jumanne.

Kama njia moja ya kuomba msamaha mashabiki waliofika siku ya Jumatatu na kumkosa msanii huyo, pallaso alikusanya baadhi ya marafiki zake na wakajipatia adhabu ya kufanya usafi kwa kufagia bara bara na mitaa yamji wa Masaka wakingoja usiku wa kutumbuiza.

Previous articleDavido Atimiza Ahadi Aliyotoa Mwaka Jana
Next articleTrey Songz: Akabiliwa Na Kesi Ya Kumingia Kinyume Mpenzi Wake
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here