Msanii na producer kutoka Bongo Flava Nahreel amejitokeza kukana madai kwamba ana mtoto wa nje ya mahusiano yake na mkewe wa sasa Aika.
Akijibu tuhuma hizo Nahreel amesema kwamba taarifa hizo zinazosambaa kwenye mitandao mbali mbali ni za uongo na zinalenga kumharibia mahusiano yake na mkewe.
Nahreel amesisitiza kwamba ana watoto wawili tu na mpenzi wake wa mda mrefu Aika ambaye pamoja wanaunda kundi la mziki la Navy Kenzo.