Jamaa mmoja kutoka maeneo ya Milore kaunti ya Kilifi amejitia kitanzi baada ya kumuua mkewe kwa kumkatakata kwa panga.
Akithibitisha kisa hicho naibu chifu wa Milore Richard Kitsao, amesema jamaa huyo kwa jina Kenga Mwanyule alimvamia mkewe kwa panga, baada ya kulumbana wakiwa njiani wakielekea katika shughuli zao za kila siku.
Baada ya kumuua mke wake jamaa huyo alijita kitanzi. Miili yao inahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Kilifi.