Msanii wa mziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Nandy amezua gumzo baada ya kufichua kwamba karibuni ameingiwa na uoga wa kufariki kupindukia.
Nandy anasema kwa mda sasa akili yake imekua ikisumbuka na fikra zinazojenga picha ya jinsi msiba wake utakavyokua iwapo atafariki leo.
Nandy majuzi alitoa video ya wimbo wake mpya kwa jina “Siwezi” ambapo kuna sehemu anaonekana akiwa kwenye jeneza akiwa amefariki.