Mama mzazi wa msanii wa Tz Diamond Platinumz kwa jina maarufu Mama Dangote amezua gumzo katika mitandao ya kijamii, baada ya kumshauri Diamond afunge ndoa na aanze familia.
Kupitia mtandao wake wa Instagram, Mama Dangote amefichua kwamba kwa sasa Diamond amepata mwanamke wa ndoto zake na hakuna chochote kinachomzuia kutofunga ndoa na kuanza familia rasmi.
Ushauri wa Mama Dangote unajiri huku tetesi zikizagaa nchini Tz kwamba kwa sasa Diamond yupo katika uhusiano mzito wa kimapenzi na msanii Zuchu, ambaye ako chini ya usimamizi wa label yake ya Wasafi.