Rapa Wizkhalifa toka Marekani ameonyeshwa kukerwa na mashabiki wenye tabia ya kumvizia kila mahali anapokwenda.
Kupitia kipande cha video kinachotrend mitandaoni, khalifa anasikika akilalamika kuwa mashabiki wanamnyima uhuru wake kama binadamu mwengine akiwasihi wamuache awe huru.
Wizkhalifa anasema mashabiki hao wamekua kero kwani wanachomfuatia nikutaka picha na yeye kila mara jambo ambalo linamnyima raha.