Msanii mkongwe wa mziki kizazi kipya kutoka Uganda Jose Chameleone amezua gumzo baada ya kujitangaza kwamba yeye ndiye msanii Bora nchini humo.
Chameleone ametaja orodha ya wasanii ambao wanafanya vizuri kwa sasa ila akaongeza kwamba hakuna miongoni mwao ambaye ameweza kufikia viwango vyake.
Kulingana na Chameleone ni kwamba wasanii ambao wamejaribu kufikia viwango vyake vya kimuziki ni Bebe Cool, Bobi Wine, Eddy Kenzo na Weasel ila bado wana kibarua Kizito kuzivunja rekodi zake.