Mchezaji Tennis maarufu duniani kwa upande wa akina dada Naomi Osaka amepinga madai kwamba amekosana na mpenzi wake wa mda mrefu kwa jina Cordae.
Mapema wiki hii kumekua na uvumi katika mitandao ya kijamii kuhusu kukosana kwao, jambo lililompelekea kuzungumzia swala hilo kupitia akaunti yake ya twitter.
Naomi amezikejeli taarifa hizo kwa kusambaza picha akiwa na Cordae wakitazama simu moja na kusema kuwa yeye na mpenzi wake pia wanazifuatailia taarifa hizo katika mitandao ya kijamii.