Kikosi cha wanasayansi wamevumbua mbinu mpya ya kutengeneza mbao katika maabara bila ya haja ya kukata mti.
Katika ripoti yao, wanasayansi wameeleza kuwa pia mbali kuvumbua mbinu ya kukuza mbao katika maabara, pia mbao hizo zinaweza kukuzwa katika muundo wowote unaotakikana na kufungua uwezo mkubwa katika swala la utumizi wa mbao kwa mahitaji tofauti ya bainadamu bila ya kukata miti na kulinda mazingira.
Wanasayansi wameeleza kuwa walitumia seli ya mti kwa jina Common zinnia (Zinnia elegans) na kuzichanganya na kemikali zengine walizotengeneza katika maabara na waligundua seli ziliongezeka na kujitengenezea mbao inayoweza kutumika kwa ujenzi.