Jamaa mmoja ameweka rekodi mpya duniani baada ya kufanikiwa kujaza upepo vibofu 10 katika kipindi cha dadika moja kwa kutumia pua badala ya mdomo.
David Rush kutoka jimbo la Idaho nchini Marekani ameingia katika vitambu vya rekodi za dunia Guinness World Record kwa kuvunja rekodi ya awali iliyowekwa na Ashrita Furman mwaka wa 2016, ambayo ilikua ni vibofu 9 kwa dakika moja.
Rush amejaza vibofu hivyo kwa kupuliza upepo kupitia pua yake kabla ya kuvifunga kwa mkono visitoe hewa iliyojazwa.