Home BURUDANI Dj Khaled Amuorodhesha “Allah” Miongoni Mwa Ma’ Producer Wakuu Wa Album Yake...

Dj Khaled Amuorodhesha “Allah” Miongoni Mwa Ma’ Producer Wakuu Wa Album Yake Mpya.

133
0

Msanii DJ Khaled wa nchini Marekani amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kubainika kwamba amemuorodhesha Mungu kama moja wapo ya watayarishi wakuu wa album yake mpya, inayotarajiwa kutoka ijumaa ya tarehe 26 mwezi Agosti 2022.

Akifichua orodha ya nyimbo zinazotengeneza album yake mpya, Dj Khaled amefichua orodha ya watayarishaji waliohusika kutengeneza album hiyo ambapo jina la Allah liwekwa kama mojawapo ya ma producer wa kuu wa album hiyo.

Akijitetea kwa uamuzi huo, Dj Khaled amedai Allah alikuwa naye studio wakati wote wa kutayarisha nyimbo za album hiyo kwa jina ‘GOD DID’ ambayo ni ya 13 katika safari yake ya mziki.

Baadhi ya mashabiki wamekerewa na uamuzi wake wakuhusisha jina la Allah katika album yake, wakieleza kuwa album hiyo ina nyimbo zinazosifu ngono na dawa za kulevya na haiwezekanai Allah alihusika kutayarisha uchafu huo.

 

Previous articleKanye West Aepuka Kesi Ya Kumshambulia Shabiki Kwa Ngumi.
Next article“Rambo” Aombwa Talaka Na Mkewe Wa Miaka 25
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here