Mkulima mmoja nchini Uigereza ameingia katika vitabu vya kumbukumbu na rekodi za dunia baada ya kufanikiwa kulima na kuvuna tangopepeta (cucumber) ambalo sasa ndio refu zaidi kuwahi kuonekana duniani.
Sebastian Suski raia wa Poland anayeishi nchini uingereza katika mji wa Southampton kwa sasa, alivuna tangopepeta lenye urefu wa futi 3 na inchi 8.6 na kuvunja rekodi ya awali ambayo ilikua ni tangopepeat la urefu wa futi 3 na nchi 6.1.
Akizungumzia mafanikio yake, Suski ameeleza kua ukulima wa kupata tangopepeta size hiyo unahitaji juhudi nyingi na umakini kwani mara nyingi linapokaa sana shambani huoza na kupasuka kabla mkulima hajafanikiwa kulivuna.