Polisi nchini Marekani wanachunguza kisa chengine wiki hii ambapo wapenzi walishikwa wakishiriki ngono uwanjani wakati wa mechi moja ya mchezo wa Baseball ikiendelea katika mji wa Toronto nchini Marekani.
Kulingana na taarifa nchini Marekani, walioshikwa walifanya kitendo hicho hadharani wakati wa mechi kati ya klabu ya Toronto Blue Jays na Chicago cubs ikiendelea.
Tukio hili ni la pili la watu kushiriki ngono uwanjani hadharani wakati mashabiki wengine wakitazama mechi baada ya kisa chengine kuripotiwa wiki iliyopita.