Home BURUDANI Kiini Cha Ugomvi Kati Ya Kanye West Na John Legend Cha Fichuliwa....

Kiini Cha Ugomvi Kati Ya Kanye West Na John Legend Cha Fichuliwa. Hutaamini!

120
0
LOS ANGELES, CA - JULY 28: John Legend and Kanye West at the Grammy Foundations Starry Night with Quincy Jones Green Room at the UCLA Tennis Center on July 28, 2007 in Los Angeles, California. (Photo by Matthew Simmons/WireImage)

 

Msanii John Legend wa nchini Marekani hatimaye amejitokeza kuzungumzia kiini cha uhasama wake na rapper Kanye West ambao umekua ukitokota kwa mda sasa.

Katika mahojiano, John Legend amefichua kuwa sababu kuu ya kununiwa na Kanye West ni hatua yake ya kutomuunga mkono katika azma yake ya kugombania urais, katika uchaguzi mkuu wa nchini Marekani ulioandaliwa mwaka wa 2020.

2020 John legend alitangaza kuunga mkono tiketi ya rais Joe Biden na makamo wake Kamala Harris katika uchaguzi huo, licha ya kuwa rafiki wa karibu wa Kanye West wakati huo akiwa anagombea kuwa rais wa Marekani pia.

John Legend ameeleza kuwa aliamua kuto muunga mkono Kanye West baada ya kuhisi Kanye West alikua anatumiwa na watu wengine ili kugawanya kura za watu weusi nchini Marekani.

Previous articleDr. Dre Na P Diddy Waingia Studio Kutengeneza Wimbo Pamoja.
Next articleMsanii The Weeknd Apoteza Sauti Yake Ghafla Jukwaani Akiendelea Kutumbuiza.
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here