Home fahamu 9 Usiyoyajua Kuhusu Malkia ELizabeth II . Nambari 4 itakushangaza!!

9 Usiyoyajua Kuhusu Malkia ELizabeth II . Nambari 4 itakushangaza!!

104
0

Anasherehekea siku za kuzaliwa mara mbili katika mwaka mmoja.

Queen Elizabeth II alizaliwa April 21, 1926 lakini umma hausherehekei siku hii hadi jumamosi ya pili ya kila mwezi Juni. Hii inachangiwa na uwepo wa hali nzuri ya anga katika mwezi wa Juni nchini Uingereza, kuwezesha raia wa taifa hilo kufanya sherehe za umma kuenzi kuzaliwa.

Hakuwahi kwenda shule.

Akiendelea kukua, Queen Elizabeth II hakupelekwa katika shule yoyote kufunzwa kama ilivyo kwa watoto wengine bali walimu waliajiriwa kumfuata nyumbani kumsomesha. Miongoni mwa masomo aliyofunzwa nyumbani ni kama vile historia ya katiba ya uingereza, sheria na lugha ya kifaransa.

Haruhusiwi kushikwa na raia wa kawaida

Sheria za Uingereza ni hatia kumgusa kiongozi wa kifalme. Hata hivyo, sheria hii inaonekana imenza kupuuzwa tangu mwaka wa 2009 wakati mke wa rais wa marekani Michelle Obama alipomkukmbatia Queen Elizabeth II alipozuru kasri lake Buckingham Palace. Wakati huo, Queen Elizabeth II alionekana kufurahishwa na hatua ya kukumbatiwa na Michelle Obama.

Alifunga ndoa na binamu wake.

Marehemu Prince Philip, Duke of Edinburgh, ambaye ndiye aliyekua mume wa Queen Elizabeth II alikua binamu wa Queen Elizabeth II. Queen Elizabeth II na Marehemu Prince Philip, Duke of Edinburgh wote ni vitukuu vya Queen Victoria. Inasemekana Queen Elizabeth II alianza kumpenda Prince Philip, Duke of Edinburgh akiwa na miaka 13, na mapenzi yao yalikua hadi walipoamua kuoana November, mwaka 1947 akiwa na miaka 21.

Queen Elizabeth II ndiye kiongozi wa kifalme Uingereza aliyetawala kwa mda mrefu zaidi.

Aliingia madarakani February 6, 1952 baada ya kifo cha babake.  Queen Elizabeth II ametawala jumla ya miaka 70 na kumpiku nyanyake Queen Victoria aliyetawala kwa miaka 63 kati ya mwaka 1837-1901.

Hauwezi kuwa mtawala wa kifalme kwa kumuoa au kuolewa na mtoto wa kifalme; iwapo atakupenda.

Kulinga na sheria za kifalme uingereza, uongozi wa kifalme hauwezi kutwika/kuambukizwa mtu mwengine na daima utafuata damu halisi ya kifalme kulingana na mpangilio wa familia ya kifalmme. Mume wa marehemu Queen Elizabeth II hakuwahi kuchukuliwa kama mfalme kiongozi bali mume tu wa malkia kiongozi wa ufalme wa uingereza.

Hahitaji Paspoti kusafiri nje ya taifa la Uingereza.

Queen Elizabeth II ndiyr raia wa pekee wa taifa hilo asiyekua na paspoti licha ya kusafiri nje ya taifa hilo.

Paspoti zote za Uingereza zinamilikiwa na Queen Elizabeth II kisheria na kutolewa kwa raia kupitia jina lake. Hii iliondoa umuhimu/haja yoyote ya yeye mwenyewe kuwa na paspoti yake binafsi. Hata hivyo watu wengine wa familia yake wanahitaji paspoti kusafiri.

Maisha ya Queen Elizabeth II yameigizwa katika zaidi ya filamu na tamthlia 200 duniani.

Amewahi kutunukiwa tuzo mwaka 2013 kufuatia mchango wake katika tasnia ya filamu, baada ya historia ya maisha yake kutumika kuandika filamu/tamthilia nyingi.

Unapokula meza moja na Queen Elizabeth II, anaposita kula kisheria unapaswa pia wewe kuacha shughuli ya kula. Hauruhusiwi kundelea kula iwapo kiongozi wa kifalme atakua ameshiba na kuacha shughuli ya kula chakula.

 

Previous articleREKODI: Atambua Bendera Za Dunia Nzima Kwa Dakika 4 Tu!
Next articleJe, haufurahishwi na kimo chako kifupi na unatamani kuongeza kimo? Amini usiamini hili linaweza kutimia kwa miezi 3!
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here