Home maajabu Je, haufurahishwi na kimo chako kifupi na unatamani kuongeza kimo? Amini usiamini...

Je, haufurahishwi na kimo chako kifupi na unatamani kuongeza kimo? Amini usiamini hili linaweza kutimia kwa miezi 3!

137
0

Kuna daktari mmoja nchini Marekani amevumbua mfumo mpya wa upasuaji ambapo unamwezesha kuongeza kimo cha binadamu.

Kevin Debiparshad, mpausaji mkuu wa hospital moja ya kibinafsi jimbo la Nevada nchini Marekani kwa jina LimbplastX Institute, amethibitisha kutekeleza upasuaji kwa wateja kadhaa na kuwaongeza urefu wao wa kimo; kwa gharama ya dola za kimarekani elfu 150, ambazo ni sawia na pesa za kenya shilingi takriban milioni 178.

Kevin ameeleza kuwa upasuaji huo unahusisha kukatwa kwa mifupa ya mapaja yote mawili na kuwekwa vyuma ambavyo vitahakikisha kuvutika polepole kwa mifupa hiyo na kupelekea kuongezeka kwa urefu wa millimita moja kila siku kwa katika kipindi cha miezi miatatu.

 

 

Mtaalamu huyo wa upasuaji ameeleza kuwa gharama ya upasuaji hiyo inaweza kuongezeka iwapo mteja atahitaji uangalizi wa kimatibabu, baada ya kukamilisha upasuaji huo huku akifichua kuwa tayari amefanikiwa kuwafanyia upasuaji wagonjwa wengi na kuwaongeza vimo vyao.

Previous article9 Usiyoyajua Kuhusu Malkia ELizabeth II . Nambari 4 itakushangaza!!
Next articleAjali: Ndege 2 Zagongana Hewani.
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here