Gavana wa jimbo la California nchini Marekani amekubali kuidhinishwa kwa sheria mpya ambapo maiti za binadamu zitakubalika kisheria kutumika kama mbolea mashambani.
Gavana Gavin Newsom ametia sahihi mswaada wa sharia hiyo na kulifanya jimbo la carlifonia kuwa la nne nchini marekani baada ya majimbo ya Washington, Colorado, Oregon na Vermont ambako maiti inayooza inaweza kutumika kama mbolea ya mimea iwapo marehemu ataagiza hivyo katika matakwa yake akiwa hai.Mfumo huu mpya umekubalika kama njia moja wapo ya kuzikana na watu ambao hawataki kuchomwa ama kuzikwa ardhini katika makaburi, wanaruhusiwa kisheria kuchagua njia na miili yao inapooza itumike kama mbolea katika sehemu wanazochagua.