Home HABARI Apigwa Ngumi Na Kufariki Papo Hapo Katika Ndondi.

Apigwa Ngumi Na Kufariki Papo Hapo Katika Ndondi.

160
0

Mwanamasumbwi mmoja amefariki baada ya kupigwa na kushindwa katika pigano nchini Colombia.

Luis Quinones wa uzito wa Welterweight alifariki akipambana na Coliseo Elias Chegwi baada ya kushindwa kwa “technical knockout” dakika moja ndani ya pambano, alipopigwa ngumi nzito ya kichwa.

Kipande cha video kinachosambaa mitandaoni kinamwonyesha Quinones akianguka katika sakafu ya ulingo na kupoteza fahamu alipopigwa ngumi, kabla ya kuondolewa katika ulingo juu ya machela.

Inasemekana alikimbizwa hospitali alikofanyiwa upasuaji wa dharura baada ya damu kuganda katika ubongo wake, lakini kwa bahati mbaya hakurudisha fahamu na kuthibitishwa kufariki na madaktari.

Previous articleUtafiti Wa Baini “Password” Inayotumika Kwa Sana Mitandaoni.
Next articleGloves Za Condom: Mtindo Mpya Wa Mavazi Ulimwenguni.
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here