Ijumaa ya tarehe 30 Septemba umma katika mji wa Taquo eneo la Palestina ulijitokeza kuomboleza kifo cha mtoto wa umri wa miaka 7, aliyeripotiwa na madaktari kufariki baada ya kuingiwa na uoga kupita kiasi.
Kulingana na ripoti ya madaktari, Rayan Suleiman alifariki baada ya moyo wake kusimama ghafla wanajeshi walipofika katika shule yao katika oparesheni moja ya kijeshi.
Madaktari wameeleza kuwa mwili wa Rayan ulitoa “adrenaline” kupita kiasi na kupelekea kugutuka kupita kiasi kwa moyo wake, uliosimama ghafla.
Mzazi wa mtoto huyo ameeleza kuwa mwanawe alikua akiogopa majeshi ya Israel kwa mda na hatua ya wanajeshi hao kuingia katika darasa lao kulimshtua kupita kiasi.