Home dunia Wizi/Udanganyifu Wa Kushangaza Zaidi Duniani

Wizi/Udanganyifu Wa Kushangaza Zaidi Duniani

110
0

1.Afungua Tawi Ghushi La Benki Ya Serikali India

Kijana mmoja kwa jina Kamal Babuu raia wa India alikamatwa na polisi baada ya kujaribu kuibia raia wa taifa hilo kwa kufungua tawi gushi la benki katika mji mmoja nchini humo.Babuu alijaribu kufungua tawi la benki moja maarufu ya India kwa jina State Bank Of India, inayomilikiwa na serikali ya India, katika mji kwa jina Panruti. Polisi walifika kumkata Babuu na wenzake wawili baada ya wananchi waliongia katika tawi hilo kuhudumiwa kuanza kushuku. Inasemekana ndani ya jengo hilo, Babuu na wenzake walikua wametengeneza na kupamba jengo hilo mithili ya benki ya ukweli.

2.Wafungua Shule Ghushi Ya Kutoa Mafunzo Ya Polisi China  

Mwaka wa 2011, Polisi nchini China waliwahi kufunga shule ghushi ya kutoa mafunzo ya polisi baada ya raia wa kutapeliwa mamilioni ya fedha wakidanganywa kwamba watajiunga na idara ya polisi ya China baada ya kumaliza mafunzo waliyolipia. Jiamusi Peoples Police Academy ndilo lililokua jina la shule hiyo iliyokua imefunguliwa katika mkoa kwa jina Shandong. Wanafunzi waliojiunga na chuo hicho feki walikua wamedanganywa watapewa mafunzo kwa kipindi cha miaka mitatau na kufuzu na degree katika maswala ya usalama wa umma, kabla ya kuajiriwa na serikali ya China.   Polisi walikutana na walimu pamoja na mamia ya wanafunzi waliokua wanaendelea na masomo walipovamia kukifunga chuo hicho.

3.Ubalozi Feki Wa Marekani Uliotoa Visa Za Ukweli Ghana

Serikali ya Ghana mwaka wa 2016 ilijipata katika aibu baada ya kugunduliwa jamaa waliokua wamefungua ubalozi gushi wa taifa la Marekani katika mji mkuu wa Ghana, Accra. Ubalozi huo ghushi ulikua ukitoa visa za mlango wa nyuma za taifa la Marekani kwa kipindi cha miaka 10 bila ya serikali ya Ghana kugundua. Ubalozi huo ulikua ukiendeshwa na mtandao wa wezi wa kimatifa waliokua katika mataifa ya Uturuki licha ya uwepo wa ubalozi halisi wa Marekani katika taifa hilo. Wafanykazi wa ubalozi ghushi walikua raia wa Uturuki na walikamatwa na zaidi ya paspoti 150 za mataifa tofauti duniani pamoja na visa feki za mataifa ya India na Afrika Kusini.

4.Auzia Benki Ya Brazil Uwanja Wa Ndege Usiokuwepo Nigeria

Raia mmoja wa Nigeria kwa jina Emmanuel Nwude alifanikiwa kuiba zaidi ya bilioni 24 mwaka wa 1998 baada ya kuuzia benki moja ya Brazili kwa jina Banco Noroeste uwanja wa ndege ambao ulikua haupo.

Emmanuel alijifanya gavana wa benki kuu ya Nigeria na kufanikiwa kumraia mkurugenzi wa benki hiyo Nelson Sagakuchi kwamba Nigeria ilikua inapanga kujenga uwanja mpya wa ndege na ilikua inatafuta wawekezaji. Benki hiyo ilitoa mamilioni ya fedha. Emmanuel alikamatwa mwaka wa 2004 na kufunguliwa mashataka 15 ya kupokea fedha kwa njia ya uongo.

5.Ajitengenezea Taifa La Uongo Na Kukusanya Ufadhili Wa Miradi Uingereza

Mwaka wa 1820 raia mmoja wa Scotland kwa jina Gregor McGregor alishangaza ulimwengu baada ya kwenda nchini Uingereza na kudanganya matajiri kwamba ni mwana wa kifalme kutoka taifa la uongo kwa jina Poyais lililopatikan katikati ya bara la Amerika. McGregor alichapisha pesa za uongo zenye sura yake pamoja ramani na kitabu cha maelezo kuhusu rasilimali za taifa lake na kurai matajiri kuwekeza fedha zao katika miradi tofauti katika taifa hilo. McGregor alifanikiwa kuibia raia wengi wa Uingereza kabla ya kuhamia taifa la Ufaransa kuibia wengine ambapo alikamatwa.

6.Ajaribu Kuuza Mnara Wa Kitaifa Wa Ufaransa (Eiffel Tower).

Jamaa kwa jina Victor Lustig, aliwahi kujaribu kuuza mnara maarufu unaotumika kutambulisha taifa Ufaransa kwa jina Eiffel Tower. Victor ambaye alikua na asili ya mataifa ya Hungary na Austria tayari alikua na kesi za awali za utapeli kabla ya kujaribu kuuza mnara huo mara mbili kwa matajiri. Mara ya kwanza Victor alidangaya matajiri kadhaa wa Ufaransa kwamba serikali ya Ufaransa ilikua inataka kuuza mnara huo kisiri kwa watu binafsi baada ya kushindwa kusimamia mahitaji yake ya kufanyiwa marekebisho ya mara kwa mara. Victor alifanikiwa kumuuzia mnara huyo jamaa mmoja kwa jina André Poisson aliyekua mwanabiashara wa kuuza vyuma vikuukuu (scrape metal) kabla ya kutorokea Austria ambako alikaa kwa mda kabla ya kurudi Ufaransa kwa jaribio lake la pili ambapo alikamatwa.

7.Ndiye Anayemiliki Mwezi Unaouona Angani Kila siku.

Mnamo mwaka wa 1980 raia wa Marekani kwa jina Denis Hope aliandikia barua umoja wa mataifa kudai umiliki halisi wa mwezi. Hii ni baada ya kusoma makubaliano ya mataifa ulimwenguni kupitia umoja wa mataifa kwamba hakuna taifa linaloweza kudai umiliki wa mwezi. Denis alitumia mwanya huo na kudai makubaliano hayo hayazuii raia wa kawaida kudai umiliki wa mwezi bali yanazuia mataifa pekee. Barua yake haijawahi kujibiwa wala ombi lake kupingwa rasmi na yeyote duniani na kuongeza nguvu madai yake ya kuwa mmiliki wa mwezi. Tangu mwaka huo amekua akidai kuwa ameuza vipande kadhaa vya ardhi ya mwezini kwa matajiri na watu maarufu ikiwemo marais. Kattika tovuti yake Hope anadai ameuza zaidi ya ekari 600 za ardhi ya mwezini kwa watutofauti duniani ikiwemo marais wa zamani wa marekani George H.W. Bush, Jimmy Carter na Ronald Reagan pamoja na watu wengine 675 maarufu duniani.

8.Adai Kuvumbua Njia ya kubadili Maji Kuwa Mafuta Ya Gari.

Mwaka wa 1980, raia mmoja wa China kwa jina Wang Hongcheng alidai kuvumbua dawa iliyokua na uwezo wa kubadilisha maji ya kawaida kuwa mafuta gari. Ijapokua hakua msomi wa maswala ya kemia, Wang alifanikiwa kudanganya idara tofauti za serikali ikiwemo jeshi la China na kupewa mamilioni ya fedha kuendeleza uvumbuzi wake. Baada ya uvumbuzi wake kutoonekana Wang alifunguliwa mashataka mwaka wa 1998 ambapo alipatikana na hatia ya udanganyifu wa kujipatia mali na kufungwa miaka 10 jela na serikali ya China.

 

 

 

Previous articleMagonjwa 9 Ajabu Zaidi Duniani
Next articleWansayansi Wagundua Njia Ya Kutabiri Kifo Cha Binadamu Kwa Kuchunguza Mwendo Wake.
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here