Home dunia Mtoto Wa Miaka 8 Afichwa Miaka 7 Bila Ya Kutoka Nje Na...

Mtoto Wa Miaka 8 Afichwa Miaka 7 Bila Ya Kutoka Nje Na Mazazi Wake.

103
0

Mama, babu na nyanya wamefunguliwa mashtaka nchini Ujerumani kwa tuhuma za kumficha binti mmoja kwa takribani miaka saba.

Kulingana na taarifa za mahakamani nchini Ujerumani, binti huyo alifichwa katika nyumba moja mji wa Attendorn mashariki mwa mji wa Cologne Ujerumani, baada ya babake kuarifiwa kuwa alisafiri nchini Italia pamoja na mamake.

Inasemekana babake alijaribu kufuatilia wanakoishi nchini Italia bila kufanikiwa, kabla ya kugunduliwa anaishi na babu na nyanyake akiwa amefichwa katika nyumba nchini Ujerumani.

Babake na mamake walikua wamekosana na mamake binti alipanga njama ya kumficha mtoto huyo kutoka kwa babake, kwa ushirikano na wazazi wake, ambao ndio baba na nyanya ya mtoto.

Mtoto huyo amepatika akiwa hajui kutembea vizuri, bila ya elimu mwanya sababu ya kutoruhusiwa kwenda shule wala kucheza na wenzake nje.

Previous articleAshikwa Airport Akijaribu Kuingia Na Bunduki Ndegeni Akiwa Amemficha Ndani Ya Kuku Mbichi.
Next articlePaka Asiyekua Na Jinsia Ya Kiume Wala Ya Kike Agunduliwa Uingereza.
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here