Makavazi kutoka jimbo la Texas nchini Marekani imefanikiwa kuchapisha kitabu ambacho kimethibitishwa kuwa kitabu kikubwa zaidi kuwahi kuchapishwa duniani.
Kitabu kwa jina “I Am Texas” chenye urefu wa saba, upana wa futi 11 na uzito wa kilo 224 kimeingia katika kitabu cha kumbukumbu za dunia cha Guinness World Record kuwa kitabu kikubwa zaidi kuhawahi kuchapishwa na binadamu.
Kitabu hicho kimechapishwa kwa ushirikiano wa ufadhili baina ya shirika moja kwa jina iWRITE na makavazi ya The Bryan Museum katika mji wa Galveston nchini Marekani.