Jamaa mmoja kwa jina Roger ‘Dean’ Gillispie kutoka jimbo la Ohio nchini Marekani amelipwa dola milioni 45 za Kimarekani ambazo ni sawia na bilioni 4.5 pesa za Kenya na mahakama nchini humo baada ya kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kimakosa.
Dean alihukumiwa miaka 56 jela baada ya mahakama kumpata na hatia ya utekaji nyara na ubakaji wa mama na binti zake mapacha mwaka wa 1991.
Hata hivyo baada ya miaka 20 ya kujitetea kwamba hakuhusika na uhalifu huo mahakamni, mwaka wa 2011 mahakama ilibatilisha uamuzi wa awali na kuamuru kuachiliwa huru kwa Dean, baada ya ushahidi mpya kutomhusisha na mashtaka.
Dean alianza mchakato wa kuishtaki serikali ya Marekani kwa kumfunga kimakosa hadi majuzi ambapomahakailiamauru allipwebilioni 4.5 kama fidia ya ufugwa kimakosa nakupotezamiaka 20 jela.