Jamaa mmoja raia wa Indonesia amegundua mke aliyeozwa siku 12 zilizopita sio wajinsia ya kike kama alivyotarajia.
Jamaa huyo aliyetambulishwa kwa jina AK mwenye umri wa miaka 26, anasemekana kufunga ndoa na aliyedhani kuwa mwanamke kwa jina Adinda Kanza majuzi kabla ya kuelekea kwa fungate.
Wawili hao wanaripotiwa kuwa katika mahusiano ya uchumba kwa kipindi cha Zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kuamua kufunga ndoa rasmi.
Inasemekana AK alianza kushuku mienendo ya Kanza baada ya kukataa juhudi zake za kufanya tendo la ndoa wakiwa fungate, jambo lilipepekea kuanzisha uchunguzi wa kisiri kubainisha kiini cha tabia zake za kushangaza.
Polisi nchini Indonesia wamelazimika kumkamata mtuhumiwa baada ya babake ya kumpata babake aliyethitisha kwamba ni mwanawe wa kiume aliyetoroka nyumbani kwao mika kadhaa iliyopita.