Home HABARI Mtoto Afariki Sababu Ya Uoga.

Mtoto Afariki Sababu Ya Uoga.

109
0

Ijumaa ya tarehe 30 Septemba umma katika mji wa Taquo eneo la Palestina ulijitokeza kuomboleza kifo cha mtoto wa umri wa miaka 7, aliyeripotiwa na madaktari kufariki baada ya kuingiwa na uoga kupita kiasi.

Kulingana na ripoti ya madaktari, Rayan Suleiman alifariki baada ya moyo wake kusimama ghafla wanajeshi walipofika katika shule yao katika oparesheni moja ya kijeshi.

Madaktari wameeleza kuwa mwili wa Rayan ulitoa “adrenaline” kupita kiasi na kupelekea kugutuka kupita kiasi kwa moyo wake, uliosimama ghafla.

Mzazi wa mtoto huyo ameeleza kuwa mwanawe alikua akiogopa majeshi ya Israel kwa mda na hatua ya wanajeshi hao kuingia katika darasa lao kulimshtua kupita kiasi.

Previous articleJoho Avaa Saa Inayogharimu zaidi ya Ksh. 45 million.
Next articleUtafiti Wa Baini “Password” Inayotumika Kwa Sana Mitandaoni.
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here