Utafiti uliofanywa na mtandao mmoja kwa jina NordPass umefichua neno la siri (password) linalotumika na watu wengi zaidi duniani mwaka wa 2021.
Kulingana na utafiti huo, 123456 ndio neno la siri linalotumika na watumizi wengi wa internet kuingia katika mitandao tofauti.
Nordpass imeonya kuwa iwapo hili ndilo neno lako la siri, itachukua sekunde moja tu kwa wadukuzi kudukua akaunti yako sababu ya urahisi wake.