Mwanamasumbwi mmoja amefariki baada ya kupigwa na kushindwa katika pigano nchini Colombia.
Luis Quinones wa uzito wa Welterweight alifariki akipambana na Coliseo Elias Chegwi baada ya kushindwa kwa “technical knockout” dakika moja ndani ya pambano, alipopigwa ngumi nzito ya kichwa.
Kipande cha video kinachosambaa mitandaoni kinamwonyesha Quinones akianguka katika sakafu ya ulingo na kupoteza fahamu alipopigwa ngumi, kabla ya kuondolewa katika ulingo juu ya machela.
Inasemekana alikimbizwa hospitali alikofanyiwa upasuaji wa dharura baada ya damu kuganda katika ubongo wake, lakini kwa bahati mbaya hakurudisha fahamu na kuthibitishwa kufariki na madaktari.