Home dunia Mji Washerehekea Kutouliwa Mtu Katika Kipindi Cha Siku Saba Mfululizo.

Mji Washerehekea Kutouliwa Mtu Katika Kipindi Cha Siku Saba Mfululizo.

83
0

Mi mmoja nchini Colombia umeshangaza watu ulimwenguni baada ya kuandaa sherehe maalum kusherehekea kupita siku saba mfululizo bila ya kuripotiwa kwa mauaji ya kihalifu.

Tangu mwaka wa 1993, mji kwa jina Medellin umekua ukijulikana na kuvuma kwa sifa ya kuwa na visa vingi vya mauji ya kihalifu; kiasi cha kwamba siku moja haipiti bila ya kuripotiwa mtu ameuliwa na wahalifu sehemu flani ya mji huo.

Mji huo umekua kitovu cha mapigano baina ya magenge ya ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Colombia; na ni mji alikotoka mlanguzi maarufu duniani Pablo Escobar. Mwaka wa 1991, kuna wakati mji wa Medellin ulishika vichwa vya habari ulimwenguni baada ya kuweka rekodi ya watu wengi kuuliwa katika siku mmoja kwa mda mrefu, ambapo ilifika hadi watu 19 kuuliwa kila siku.

Majuzi mji huo umefanikiwa kutimiza wiki moja (siku saba) bila ya mtu kuripotiwa kuuliwa na kupelekea kuandaliwa kwa sherehe maalum katika mji huo, kuadhimisha mafanikio hayo.

Hata hivyo, uwepo wa usalama uliopelekea sherehe hiyo unasemekana sio sababu ya kazi nzuri ya polisi wa mji huo, bali makubaliano baina ya magenge tofauti ya ulanguzi wa dawa za kulevya pamoja na polisi, kuhusu kuhakikisha kutokeupo kwa uhalifu katika maeneo magenge yanatawala kibiashara.

Mji gani huezi kuishi hata uambiwe nini!! unaogopa sababu ya sifa zake umeskia ama kuna kisa kilikupata?

Previous articleDaktari Mzee Zaidi Duniani Anayendelea Kutibu Wagonjwa.
Next articleMagonjwa 9 Ajabu Zaidi Duniani
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here