Maafisa wa wanyama pori katika makao ya wanayma pori jimbo la Colorado nchini Marekani wamegonga vichwa vya habari baada ya kufichua kuwa kumezuka tabia ya watu wanaotemebela wanyama katika makao hayo kuramba kwa ndimi zao aina flani ya chura anayehifadhiwa katika makao hayo.Katika taarifa kwa umma ambayo imeshangaza watu, The National Parks Service nchin Marekani imefichua kuwa kuna watu hutembea kumuona chura mmoja aina ya Sonoran Desert toad makao hayo na kumlamba wanapopewa kumshika ili kumuangalia.