Home dunia Amea Pua Mkononi Akipambana Na Saratani

Amea Pua Mkononi Akipambana Na Saratani

128
0

Mwanamke mmoja nchini Ufaransa aliyepoteza pua yake katika upasuaji wa kupambana na saratani ya pua amefanikiwa kujitengeneza pua mpya kwa kuikuza upya katika mkono wake.

Mwanamke huyo aliyetambulishwa kwa jina moja la Carine, alikatwa pua yake na madaktari mnamo mwaka wa 2013, wakati alipogunduliwa kuugua na saratani ya sinus iliyokua imeshinda kutibika.

Baada ya upasuaji wa kuondoa pua yake kuokoa maisha yake, Carine alishindwa na kujitokeza mbele ya watu sababu ya aibu ya kutokua na pua katika sura yake na pia alipata matatizo kwa kukosa uwezo wa kunusa ama kuskia harufu ya vitu tofauti katika maisha yake.

Majuzi madaktari walimpa mbinu ya kukuza pua mpya kutumia nyama katika mkono wake.

Katika mpango huo kifaa kilichochongwa mfano wa pua ya binadamu kiliingizwa na kushonwa chini ya ngozi yake katika sehemu ya mkono, ili seli na mishipa ya damu imee katika mundo wa pua.

Kwa kipindi cha wiki mbili, pua ilkua imekamillika kujitengeza na ilikatwa na kupandikizwa katika uso wake na kurudisha sura kamili ya binadamu wa kawaida

katika upandikizi wa pua, madaktari walishona na kuunganisha mishipa ya damu ya sura na pua mpya ili ifanyekazi kamakawaida.

Previous articleTunazaana Sana: Idadi Ya Binadamu Duniani Imefikia Bilioni 8 Sasa.
Next articleWanasayansi Wagundua Panya Wanacheza Mziki Kama Binadamu
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here