Home HABARI Jamaa Aliyefungwa Jela Miaka 214 Achiliwa Huru

Jamaa Aliyefungwa Jela Miaka 214 Achiliwa Huru

113
0

Jamaa mmoja aliyekua amehukumiwa kifungo cha miaka 214 jela nchini Marekani hatimaye ameachiliwa huru baada ya kutumikia jela miaka 27 tu.

Bobby Bostic, ambaye kwa sasa ana miaka 43, aliachiliwa huru chini ya sheria ya jimbo la Missouri ambapo mtu anaweza kusamehewa kifungo chake, iwapo alihukumiwa kufungwa jela na Mahakama akiwa mtoto (chini ya umri wa miaka 18.)

Bostic alifungwa jela akiwa na umri wa miaka 16 baada ya kupatikana na hatia ya kosa la wizi wa mabavu katika mji wa St Louis ambapo watu wawili walifariki.

Kulingana na rekodi za mahakama iwapo haingekua sheria hiyo kuhusu watoto waliofungwa ombi la kusamehewa la Bostic lingefaa kusikizwa mwaka wa 2201 ambapo wengi wetu hatungekua hai duniani.

Inasemekana msahama huo umekuja baada ya Bostic kuonyesha kuwa na tabia njema akiwa jela, ambapo inasemekana aliweza kusoma hadi kufuzu na shahada ya degree mbali nakuandika jumla ya vitabu 15.

Previous articleWanasayansi Wagundua Panya Wanacheza Mziki Kama Binadamu
Next articleAshikwa Na Polisi Baada Ya Kujirekodi Akila Popo Mtandaoni
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here