Home HABARI ARDHI TANA

ARDHI TANA

61
0
Tana River (photo courtesy)

Gavana wa kaunti ya Tana River Dhadho Godhana amesema mpango wa vijiji vya kisasa ndio utakaokuwa suluhu ya mpangilio wa ardhi ya kaunti hiyo.

Godhana amebainisha kuwa, katika mpango huo kutatengwa sehemu mbali mbali kama vile sehemu za kuzikana, makazi na sehemu za maabadi.

Gavana huyo amesema hayo baada ya waumini wa dini ya kiislamu kutoa ombi la kutengewa sehemu zaidi za kuzikana kwa sababu ya ongezeko la watu mjini Hola.

Wakati uo huo mbunge wa Galole Said Buya Hiribae amewahakikishia wakazi kuhusu kuweka msukumo zaidi bungeni ili mji wa Hola upate ardhi ya kutosha kwa maendeleo ya mji.

Hiribae amesema tayari aliwasilisha hoja bungeni ya kutaka mamlaka ya unyunyizaji ya Hola kukabidhi serikali ya kaunti hiyo maelfu ya ekari ya ardhi na badala yake mamlaka hiyo kupewa ardhi iliyo mbali na mji.

Previous articleApigwa Risasi Na Mbwa Wake Na Kufariki Papo Hapo
Next articleKANU YAKASHIFU
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here