Home HABARI MAZISHI TANA

MAZISHI TANA

50
0
Dhado Godana (photo courtesy)

Gavana wa kaunti ya Tana River Dhadho Godhana amejitenga na madai kwamba ameidhinisha mwanasiasa atakayemrithi katika uchaguzi wa mwaka 2027.

Akiongea katika hafla ya mazishi ya msomi na mwanasiasa aliyegombea uwakilishi wa wanawake kaunti hiyo Dkt. Medina Halako Twalib, Godhana anasema hajaidhinisha yeyote wa kumrithi, akisema jamii yenyewe ndiyo itakayoamua.

Amesema hayo huku akimsifu mwenda zake akisema alikuwa mwanamke wa kwanza msomi kaunti hiyo aliyepata PhD akiwa na miaka 33 pekee kabla ya kuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Nairobi kwa miaka 5.

Viongozi wa kisiasa waliohudhuria mazishi hayo wakiongozwa na aliyegombea ugavana kaunti hiyo uchaguzi uliopita Ali Wario wamemsifu Halako kwa msukumo wake wa kumaliza ukabila kaunti hiyo.

Hayo yanajiri huku wengi wao wakimtaka gavana Godhana kuipa jina lake moja ya barabara za mjini Hola kuwa kumbukumbu yake.

Previous articleKANU YAKASHIFU
Next articleWANAHARAKATI MAFUNZO
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here