Wanainchi huko Kirinyaga wamemkamata afisaa mmoja wa polisi na kumpeleka katika kituo cha polisi, baada ya kudai hongo kutoka kwa wafanyibiashara.
Kulingana na mfanya biashara mmoja kutoka Gilgil kwa jina Nathan Wangui Ndirangu ni kwamba afisaa huyo amekua akiitisha 2000 kwa wafanya biashara wanaofungua biashara zao mda wa curfew licha ya sheria ya curfew kuondolewa.
Afisaa huyo alikamatwa katika soko la Kagumo na wanainchi na wakambeba moja kwa moja hadi kwa kituo cha polisi cha Kagumo. Afisaa huyo wa polisi kwa sasa anashikiliwa na polisi akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya ufisadi.