Home BURUDANI Wasanii Pwani Watetea Utumizi Wa Fedha Za Kaunti Kuwalipa kwa Sherehe

Wasanii Pwani Watetea Utumizi Wa Fedha Za Kaunti Kuwalipa kwa Sherehe

130
0

Wasanii wa mziki wa kizazi kipya kutoka kanda ya pwani wamepinga vikali madai kwamba walilipwa shilingi milioni 200 na serikali ya Mombasa katika tamasha la mziki la kufunga mwaka lililofanyika katika bustani ya Mama ngina wakati wafanyikazi wa kaunti ya Mombasa walikua hawajalipwa miezi 3 mfululizo.

Baadhi ya wasanii waliotumbuiza kwenye tamasha hilo wanadai kiwango wanachodaiwa kutumika katk auandalizi wa tamasha hilo sio cha ukweli na kinalenga kuiharibia jina serikali ya kaunti ya Mombasa.

Kwa upande wake mmoja ya waandalizi watamasha hilo msanii Susumila ameeleza kwamba wasanii waliotumbuiza katika tamasha hilo bado kufikia sasa hawajapokea malipo yao kamili kinyume na madai ya watu.

Previous articleDiamond atangaza kumrudisha Queen Darling
Next articleKasisi Afutwa Kazi Kisa Hajapata Mke
Teddy Mwanamgambo is a media personality in the coast region. He has worked in different media houses over a period of time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here