Waumini wa kanisa la ACK huko Othaya kaunti ya Nyeri wameandamana kulalamikia kasisi wao kufutwa kazi kisa hajaoa.
Kulingana na waumini hao ni kwamba kasisi huyo kwa jina Joseph Kagunda anayeongoza dayosisi ya mlima Kenya mashariki aliachishwa kazi na uongozi wa kanisa la Anglican kwa sababu hajaoa.
Uongozi wa kanisa hilo unasema ulimpa miezi sita kasisi huyo kutafuta mke aoe lakini alishindwa.
Waumini wa kanisa hilo walienda hadi nyumbani kwa kasisi huyo na kuandamana naye moja kwa moja hadi kanisani kwa lazima ili awaongoze kwenye ibada wakihoji kwamba kumpata mke sio kitu rahisi kama kununua bidhaa dukani.