Msanii Bebe Cool kutoka Uganda amezua gumzo baada ya kudai kwamba hakuna msanii mkubwa zaidi yake yeye na msanii mwenza Jose Chameleon katika taifa hilo.
Bebe Cool anadai yeye pamoja na Chameleon wana mchango mkubwa kwenye tasnia ya mziki wa taifa hilo kuliko msanii yoyote mwingine mbali na kutoa hits nyingi ambazo zimeutangaza mziki wa Uganda kimataifa tangu waingie kwenye mziki.
Wawili hao wanatarajiwa kutoana kijasho kwenye tamasha moja mjini Nambole, kupimana nguvu nani mkali baina ya wawili hao.