Polisi huko Kiamisiori kaunti ya kisii wanawatafuta ndugu wawili baada ya kumuua baba yao mzazi kwa kumkatakata kwa slasher na kisu.
Kulingana na Ripoti ya DCI eneo hilo ni kwamba wawili hao Boniface Osoro pamoja na kakake Getaro Osoro walitokomea kusikojulikana baada ya kutekeleza kitendo hicho.
Majirani kwa upande wao wanasema walimskia mzee huyo akipiga kamsa ndipo walipoamua kufika kumsaidia ila ila juhudi zao ziliambulia patupu kwani walifika kumpata mzee huyo akikata roho.
Hadi sasa haijajulikana sababu rasmi ya wawili hao kutekeleza kitendo hicho cha kinyama huku shughuli ya kuwatafuta ndugu hao wawili likiendelea.