Polisi huko Uganda wanawashikilia watu wa tatu baada ya kumuua mwenzao kisa deni la pombe la shilingi 32.
Kulingana na taarifa ya polisi wilaya ya Rukugiri mwanaume huyo kwa jina Fred Obadiah aliingia kwenye mkahawa mmoja na kuagiza Pombe ya bei ya shilingi 1000 za Uganda ambazo ni sawia na shilingi 32 za kenya na kuchomoka bila kulipa.
Inaripotiwa wahudumu walipiga kamsa ya mwizi ambapo watu waliokua nnje walimshambulia hadi kumuua.